UGONJWA USIOJULIKANA WAIBUKA KAGERA

Ugonjwa ambao bado haujajulikana ubeibuka mkoani Kagera ambao unadaiwa kuua watu watano.

Taarifa iliyotolewa jioni hii na Wizara ya Afya imesema serikali imepata habari hizo na tayari imetuma timu ya wataalamu kuona ni nini tatizo huku sampuli za waliopoteza maisha na wagonjwa zikichukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Wakati serikali ikifanya hivyo, imetoa tahadhari kwa wananchi kuhakikisha wanakaa mbali na wagonjwa hao na kutoa taarifa mara moja kwa vituo vya afya wanapobaini wagonjwa wa aina hiyo.

Aidha, imewataka wananchi endapo itabidi kuwapa huduma ya kwanza wagonjwa hao, kuhakikisha hawajichanganyi kwa kushea damu, jasho, mate na wanaohisiwa kuwa wagonjwa wa ugonjwa huo.

No comments