TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YAPANIA KUJENGA MAKUMBUSHO YA KITALII DODOMA
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Paul Kimiti, amesema endapo watapewa ardhi waliyoiomba kwa serikali, wamepania kujenga makumbusho ya muasisi huyo wa taifa ambayo pia yatakuwa kivutio cha utalii mkoani Dodoma.
Mzee Kimiti ameiambia Ojuku Blog kuwa makumbusho hayo licha ya kubeba sanamu za kiongozi huyo na wanaharakati wenzake, pia wanalenga kutengeneza bustani, shamba darasa ambalo ni kielelezo cha kuthamini kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hili.
Aidha, alisema wanakusudia pia kujenga kumbi za mikutano, viwanja vya michezo mbalimbali na maeneo mengine mengi ambayo yatamfanya mtu anayetembelea makumbusho hayo asitamani kutoka.
Alisema bado wako katika mazungumzo na serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo hasa wahusika wa malengo yao ya kuitengeneza makumbusho hayo ya kitalii.

Post a Comment