KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA BANDARI YA KAREMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),  Mhe. Jerry Silaa (wa tano kulia) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo na Sehemu ya Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mara baada ya kamati hiyo kutembelea bandari ya Karema Mkoani Katavi.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Juma Kijavara akifafanua jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kuhusu mipango ya TPA kwa bandari ya Karema, wakati kamati hiyo ilipotembelea bandari hiyo Mkoani Katavi.


Muonekano wa Bandari ya Karema baada ya ujenzi wake kukamilika. Ujenzi wa Bandari hiyo umegharimu takribani bilioni 47.9 na inatarajiwa kuhudumia mzigo mkubwa unaozalishwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia.





No comments