RAIS WA CHINA AJITOSA KUSULUHISHA URUSI, UKRAINE, MAREKANI YABEZA
Rais Xi Jimping wa China atasafiri kuelekea Moscow Machi 20 mwaka huu, kwenda kukutana na swahiba wake Vladimir Putin katika jitihada za kumaliza vita kati yake na Ukraine.
Tayari maofisa wa ngazi ya juu wa nchi hiyo wamezungumza na wakubwa wa Ukraine juu ya suala hilo na wamebariki hatua hiyo.
Hata hivyo, White House, Ikulu ya Marekani imebeza jambo hilo ikidai China imekataa kushutumu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ikikubaliana na Urusi kuwa huo sio uvamizi bali ni operesheni maalum ya kijeshi.
China, rafiki wa nchi zote mbili za Urusi na Ukraine, imekataa kuwa na upande katika mzozo huo, ikisema ni meza pekee ndiyo inaweza kupata suluhisho kwa faida ya pande zote.

Post a Comment