MWANAFUNZI APOTEZA MAISHA AKITUMIKIA ADHABU YA KUONGEA KISWAHILI SHULENI
Wakati Tanzania ikipiga upatu wa kutaka Lugha yake ya Taifa ya Kiswahili isambae na kutambuliwa duniani, mwanafunzi wa kidato cha kwanza amefariki wakati akitekeleza adhabu aliyopewa na mkuu wa shule kwa kosa la kuongea lugha hiyo shuleni!
Glory Faustine aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari Mwinuko, iliyopo Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza aliangukiwa na gema la udongo wakati akitumikia adhabu hiyo, kwa kile kilichoelezwa kuwa kiswahili hakiruhusiwi kutumiwa na wanafunzi shuleni hapo.

Post a Comment