RAIS SAMIA AWAAMBIA CHADEMA HAWANA DHAMIRA YA KUSHIKA DOLA 2025
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ulioandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), unaofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi leo.
Aliwaaambia wanawake hao wa Chadema kuwa anafahamu kila mwanasiasa ana nia ya kushika dola, hivyo akawataka kwenda kufanya siasa za kistaarabu, ili kulinusuru taifa lisije kurejea kule lilikotoka kwani kwa kipindi kifupi limepata heshima kubwa duniani.
Awali Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alimtahadharisha Rais Samia kukaa mbali na watu wanaojiita chawa, kwani siku zote hawana nia njema na nchi, isipokuwa wanataka kulinda na kutetea masilahi yao binafsi.


Post a Comment