RAIS SAMIA ASEMA SUALA LA AKINA MDEE LIACHIWE MAHAKAMA
Rais Samia suluhu Hassan ametaka suala la wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliojiteua na kujitangaza kwenda bungeni bila ridhaa ya chama hicho, kuachiwa mhimili wa Mahakama ili sheria ichukue mkondo wake.
Rais Samia alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ulioandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) uliofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Awali, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaka Rais Samia kutowalipa mshahara wabunge hao, akidai walifanya uhuni wakati wa mchakato
wa kuelekea bungeni.


Post a Comment