RAIS SAMIA ATUNUKIWA NISHANI YA JUU YA HESHIMA AFRIKA KUSINI LEO
Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo katika ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini, leo ametunukiwa Nishani ya Juu ya Heshima na kiongozi wa taifa hilo kubwa barani Afrika, Cyril Ramaphosa.
Nishani hiyo, The Order Of South Africa, imetolewa kwa mama kwa kutambua mchango wake katika siasa za Afrika, lakini pia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuchukua urais wa Tanzania.
Aidha, amepewa nishani hiyo kwa taifa hilo la kusini mwa Afrika, kutambua mchango wa Tanzania Kijeshi, kisiasa na kiuchumi, kwani kwa muda wote tangu miaka ya 1960, wapigania uhuru wa Afrika Kusini waliitambua Tanzania kama nyumbani.
Mama yupo bondeni kwa ziara ya kiserikali na Rais Ramaphosa amesema daima, nchi yake inajivunia uhusiano wa nchi mbili hizi.

Post a Comment