KOCHA MBELGIJI APONDA WANAOPOTOSHA KUHUSU FIFA KUIFUNGIA YANGA

Aliyewahi kuwa Kocha wa Yanga, Luc Eymael ameponda vikali kauli na maandiko yanayoandikwa mitandaoni kuhusu suala lake na klabu hiyo ya Jangwani, wakiihusisha FIFA.

Watu waliandika mitandaoni jana kuwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeifungia klabu ya Yanga kutosajili kwa madirisha matatu kwa kushindwa kumlipa Eymael haki zake.

Lakini kocha huyo raia wa Ubelgiji ambaye Yanga ilivunja naye mkataba baada ya kutoa lugha ya dharau kwa mashabiki, ameibuka na kusema habari hizi hazina ukweli, isipokuwa hilo linaweza kutokea endapo hatalipwa stahiki zake kwa wakati.

Amesema FIFA imetoa siku 45 ili awe amelipwa haki zake kiasi cha zaidi ya dola 90,000, lakini endapo hilo halitafikiwa, basi mabingwa hao wa nchi, wanaweza kukabiliwa na adhabu, ikiwemo ya kufungiwa kusajili.

No comments