MZEE KIMITI ASEMA RAIS SAMIA AMETHIBITISHA WANAWAKE WANAWEZA

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Paul Kimiti, amesema utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan amethibitisha pasipo shaka kuwa wanawake wanaweza.

Akiongea na Ojuku Blog kuhusu maoni yake ya siku ya wanawake duniani yanayoadhimishwa leo, Mzee Kimiti alisema Rais Samia ameonyesha weledi mkubwa wa uongozi hasa falsafa yake ya Kazi Iendelee, akisema hiyo ni kuenzi kazi zilizofanywa na watangulizi wake katika nafasi ya urais kuanzia Mwalimu Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli.

"Hakutaka kuja na slogan mpya, yeye anataka kazi zote zilizoanzishwa na watangulizi wake ziendelee. Katika miaka yake miwili ya uongozi, amefanya vitu vingi na vingine vikiwa ni nje kabisa ya bajeti. Huo ni ujasiri wa hali ya juu na anaendelea kupambana na maadui watatu wakubwa ambao ni umasikini, ujinga na maradhi."


Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo mkongwe amesema kitendo cha Rais Samia kuendelea kuteua wasaidizi wake, kinaonyesha wazi kuwa hajapata watu wanaoweza kwenda na kasi yake ya uongozi.




No comments