RAIS SAMIA ALA TANO KWA KUIFUNGUA NCHI KIMATAIFA
Akielekea kutimiza miaka miwili tangu aingie madarakani, Rais Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kitendo chake cha kiifungua nchi kimataifa, kwani hivi sasa kuna uhusiano bora zaidi kati ya Tanzania na mataifa mengine ulimwenguni.
Pongezi hizo zimetolewa na viongozi wa Kamati ya Amani na Jumuia ya Maridhiano Tanzania, Shehe Alhadi Salum ambaye alisema katika kipindi cha miaka miwili, Rais Samia amefanya mambo mengi makubwa na mazuri.
Aliyataja mambo hayo ni pamoja na kukuza uhusiano wa kimataifa, kurejesha demokrasia iliyotoweka na ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo itachangia kukuza uchumi wa Tanzania.

Post a Comment