HARMONIZE AKOLEZA VITA VYAKE NA DIAMOND, SASA ATAFUTA MAWAKILI AENDE MAHAKAMANI
Msanii kiongozi wa lebo ya Konde Gang, Harmonize ambaye kwa muda sasa amekuwa akimlalamikia bosi wake wa zamani Diamond Platnumz kuhujumu mapato yake, anatafuta msaada wa kisheria ili kulifikisha suala hilo mahakamani.
Mkali huyo wa kibao cha Single Again, anadai Diamond kupitia kampuni yake ya Wasafi, amekuwa akishirikiana na kampuni ya usambazaji muziki ya Mziiki kuhujumu mapato yake kwani yanaingia katika kampuni ya Wasafi wakati alishaachana na lebo hiyo miaka mitatu iliyopita.
Licha ya kuwatafuta mawakili wa kumsaidia kisheria, pia msanii huyo amemuomba Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ambaye pia ni rapa, kumsaidia ili apate haki yake.

Post a Comment