JAY Z HATAKI HELA KUSHIRIKI KOLABO, ANAJALI HESHIMA

Mwanamuziki nyota na tajiri wa muziki nchini Marekani, Jay Z, amesema hatozi kiasi chocbote cha fedha ili kushirikiana wimbo na msanii ye yote, bali anachojali ni heshima.

Jigga ambaye ni miongoni mwa wasanii matajiri zaidi duniani, alisema licha ya heshima, kitu kingine anachojali ni kile kilichomo kwenye wimbo wa msanii husika.

Jay Z alikuwa ameulizwa yeye pamoja na milionea mwingine Kanye West, juu ya kiwango cha fedha wanachowatoza wasanii wanaohitaji kuwashirikisha katika nyimbo zao.

Imekuwa ni kawaida kwa wasanii wakubwa kutoza fedha ili washiriki kolabo kwa kile wanachoamini wimbo watakaoshiriki utakuwa mkubwa na wenye kufuatiliwa na mashabiki katika platforms mbalimbali.

No comments