RAIS RUTO ANYOOSHA MIKONO, ATAKA MAZUNGUMZO NA RAILA
RaisvWilliam Ruto wa Kenya ambaye amekuwa na misimamo mikali dhidi ya mpinzani wake mkubwa kisiasa Raila Odinga, hatimaye amelegeza na kusema yupo tayari kwa mazungumzo.
Hata hivyo, Ruto amesema atakaa na viongozi hao kama tu ajenda yao italenga kumsaidia mwananchi wa kawaida wa Kenya na siyo matakwa yao binafsi.
Raila anayeongoza muungano wa Azimio, amekuwa akisisitiza kuwa hautambui uchaguzi mkuu uliopita akidai kuibiwa kura, lakini pia akisema serikali haijali kupunguza maisha magumu yanayowakabili wakenya.
Akiwa katika ibada ya Jumapili, Rais Ruto alisema hakuna mtu anayeweza kumshinikiza kukutana na viongozi wenye ajenda binafsi, lakini kwa manufaa ya nchi yao, yupo tayari kusikiliza.
Viongozi mbalimbali wa dini, akiwemo Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini humo, Phikip Anyollo wamekuwa wakitaka viongozi hao wa kisiasa kukaa pamoja na kusikilizana.
Wakati Ruto akitoa kauli hiyo, Raila alisema mazungumzo yanaweza tu kufanyika baada ya maandamano ambayo yamepangwa kufanyika leo kote nchini Kenya.

Post a Comment