TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA LEO NA KESHO

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa tahadhari kuwa mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika baadhi ya mikoa nchini hasa leo na kesho.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imeitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani pamoja na kisiwa cha Mafia.

TMA imesema miongozi mwa athari zinazoweza kutarajiwa ni pamoja na baadhi ya makazi ya watu kuzungukwa na maji na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi.

No comments