MAANDAMANO YAKAMATISHA 20 KENYA, VURUGU ZATAWALA MJI MKUU NAIROBI
Raia wa Kenya wameitikia wito wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa kuingia barabarani kupinga kupanda kwa gharama za maisha na kushuka kwa thamani ya sarafu yao kufananisha na dola ya Marekani, huku watu 22 wakiripotiwa kukamatwa.
Polisi nchini Kenya ilizuia maandamano hayo wakisema hayakufuata utaratibu, lakini viongozi wa upinzani walifanikiwa kupenya na kuingia KICC, sehemu ambayo ilipangwa kuanzia maandamano hayo.
Wakazi wengi wa Nairobi waliingia mtaani, lakini askari walitumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya na kuwakamata baadhi yao.
Katika kitongoji cha watu fukara zaidi jijini Nairobi cha Kibera, baadhi ya waandamaji walisema waliahidiwa kushuka kwa bei ya unga, lakini imwkua uongo.
Licha ya kupanda kwa gharama za maisha, Kenya pia imeshuhudia ukame mkubwa kufuatia kutonyesha kwa mvua kwa miaka kadhaa sasa.

Post a Comment