NDOA YA DAVID KAFULILA YAVUNJWA NA MAHAKAMA

Ndoa ya mwanasiasa machachari, David Kafulila na aliyekuwa mkewe, Jesca Kishoa, iliyofungwa April 22, 2014 imevunjwa rasmi na Mahakama.

Kituo Jumuishi Huduma za Kimahakama, Mirithi na Ndoa, imetoa hukumu ya kuivunja ndoa hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa haiwezi kurekebishika.

Katika uamuzi huo wa mahakama uliotolewa Februali 20 mwaka huu, wawili hao watawajibika kwa matunzo ya watoto wao, kila mmoja kwa asilimia 50 na kwamba kwa sasa, watakuwa chini ya uangalizi wa mama yao.

Wawili hao, ambao wote ni wanasiasa walitengana tangu mwaka 2019 kwa matatizo ambayo hayakuweza kupatiwa uvumbuzi na wawili hao hadi mahakama ilipotoa hukumu hiyo.

No comments