FATMA KARUME KUMSHAURI FEI TOTO AENDE CAS

Fatma Karume, mmoja kati ya wanasheria machachari wa kike nchini, ambaye juzi alimuwakilisha kiungo Feisal Salum katika mapitio ya hukumu yake katika Shirikisho la soka nchini TFF, amesema atamshauri mwanasoka huyo kukata rufaa ya hukunu yake katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo ya Kimataifa CAS.

Hiyo ilikuwa ni baada ya Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya TFF kukazia hukumu yake ya awali kuwa mchezaji huyo aliyevunja mkataba na klabu yake, bado ni mchezaji wa Yanga.

Wakili Fatma alisema kama Fei Toto alithibitika kuvunja mkataba kinyume na makubaliano, alipaswa kupigwa faini badala ya kulazimishwa kufanya kazi na Yanga.

"Sheria za FIFA zinasema mkataba ukivunjwa bila kufuata utaratibu,mkosaji anapaswa kupigwa faini na siyo kumlazimisha kufanya kazi na mtu ambaye hamtaki."

Alisema endapo TFF itaendelea kumlazimisha kuichezea Yanga, atamshauri kulipeleka suala lake CAS.

No comments