NATO YAKIRI URUSI INAKARIBIA KUUTWAA MJI WA BAKHMUT

Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi (NATO), umekiri kuwa jeshi la Urusi linalopambana na Ukraine, linakaribia kuutwaa mji muhimu wa kimkakati kivita wa Bakhmut.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg ambaye alizungumza na waandishi wa habari jijini Stockholm Sweden, alisema Ukraine inahitaji msaada zaidi wa kijeshi maana siku chache zijazo, Urusi itautwaa mji huo ambao umezingirwa.

Bakhmut, mji ambao ulikuwa na wakazi wapatao 70,000 kabla ya vita, hivi sasa umeharibiwa vibaya na hakuna jengo ambalo halijaguswa na bomu na karibu wakazi wote wameukimbia mji huo.

Vita hivyo vilivyoanza mwaka jana, vimeingia katika mwaka wake wa pili na hakuna dalili za mvutano huo kumalizika kwa mazingumzo.

No comments