MATAIFA AFRIKA MASHARIKI YACHACHAMAA ISHU YA MASHOGA
Ghafla, ishu ya ushoga na mashoga imepata wakati mgumu kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, viongozi wake wakija juu kukataa suala hilo kuhalalishwa katika mataifa yao.
Alianza Yoweri Museveni, akitangaza serikali yake kutovumilia suala hilo na akishangaa inakuaje mwanaume kumvutia mwanaume mwenzake.
Uganda inapeleka muswada bungeni ambao unapendekeza adhabu kali kwa wafadhili, wachapishaji wa vitabu vya uhamasishaji ushoga, wamiliki wa hoteli wanaowapangisha wapenzi wa jinsia moja na wengine wote wanaoupa msukumo ujinga huo.
Nchini Kenya, Rais Ruto ametoa msimamo wa nchi yake kutoruhusu ushoga, kama ambavyo Zambia nayo imesisitiza jambo hilo halitapewa nafasi nchini humo.
Kule Burundi, watu 24 wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Mapenzi ya jinsia moja yamekuwa wakipigiwa upatu na mataifa ya Ulaya kwa kigezo cha haki za binadamu na baadhi ya mikopo inayotolewa kwa baadhi ya nchi huambatana na masharti ya kutimiza haki za bibadamu, ikiwemo kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.

Post a Comment