H BABA ATOA MPYA, AKIRI MAISHA YAKE YANAMTEGEMEA MUNGU NA DIAMOND

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Hamis Ramadhan maarufu kama H Baba ametoa ya moyoni baada ya kuandika waraka mrefu katika akaunti yake ya Instagram, akimsifia staa Diamond Platnumz kuwa ukiondoa Mwenyezi Mungu, kijana huyo kutoka Tandale ndiye anayemfanya aishi.

H Baba ambaye aliwahi kudai kuibiwa kama si wimbo basi beat za wimbo wa Nataka Kulewa wa Diamond, alisema bosi huyo wa Wasafi ana roho nzuri na ya kusaidia wenzie, ambayo anaamini wengi hawana.




Alisema bosi huyo wa lebo ya WCB licha ya kumfanikishia ubalozi ambao analipwa shilingi milioni nne kwa mwezi, pia amempatia safari ya kimuziki nchini Marekani katikati ya Mei mwaka huu.

"Ni vijana wachache wanaweza kuwa na moyo huu, wangekuwa wengine wangetupa taabu sana hapa mjini, lakoni nashukuru, familia yangu ya Dar na Mwanza inaishi vizuri sababu yake".

No comments