NAHODHA WA HOROYA ATAMBA KUWASHANGAZA SIMBA JIONI HII KWA MKAPA

Kuanzia saa moja usiku leo Jumamosi, kikosi cha Simba kitaingia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwavaa Horoya Fc ya Guinea katika mchezo utakaoamua hatima yao kuelekea robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu.

Endapo wataibuka na ushindi watakuwa wamekata tiketi ya kusonga mbele lakini endapo watapoteza, itakuwa imekula kwao kwa vile mchezo wao wa mwisho utakuwa mgumu ukipigwa ugenini wakati wapinzani wao watakuwa na mchezo mwepesi utakaochezwa nyumbani.

Lakini Ocamsey Mandela ambaye ndiye nahodha wa Horoya, ametamba kwamva wanakuja kuwafunga Simba kama ambavyo wamefungwa na timu zingine katika uwanja wao.

Alisema licha ya kuwaheshimu wapinzani wao hao, lakini hawawezi kusafiri toka kwao kisha waje wapoteze mchezo.

No comments