ACHA ZILE ZA MAMA, WACHEZAJI SIMBA KUKUNJA MILIONI 250 WAKIMCHINJA MTU
Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba jana jioni iliwatembelea wachezaji wake walio kambini Mbweni na baada ya kula nao chakula cha usiku, wakatoa ahadi ya kuwashikisha shilingi milioni 250 endapo watampiga mtu dimbani Benjamin Mkapa jioni ya leo.
Habari zilizothibitishwa na bosi wa benchi la ufundi, zimesema wachezaji wote wana morali wa hali ya juu na Nahodha John Bocco akaahidi watapambana kufa na kupona kuipeleka timu robo fainali.
Mzigo huo, ni tofauti na ule alioahidi Rais Samia kwa kila goli kulinunua kwa shilingi milioni tano.

Post a Comment