MBOWE ASEMA NI UPOFU KWA TANZANIA KUAMINI MADINI NA MBUGA NI UTAJIRI

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema ni upofu kwa nchi kuamini kwamba sisi ni matajiri kwa kuhesabu kiasi cha madini na mbuga za wanyama au maliasili zingine zilizopo kama utajiri.

Badala yake, amesema taifa linapaswa kujikita katika kutoa elimu kwa watu wake ili wajitambue, kwani hilo likifanyika ni rahisi kwa rasilimali hizo kuweza kuwasaidia.

Mbowe alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu jana.

Alisema mataifa yote yaliyoendelea yamewekeza elimu kwa watu wao, ndiyo maana yamezidi kuendelea.

Aidha kuhusu mazungumzo ya maridhiano yanayoendelea, Mbowe alisema wanaangalia sheria za uchaguzi na tume huru ya uchaguzi miongoni mwa mambo mengi yanayoangaliwa.

No comments