MAMA SAMIA ATAKA YANGA WATUPIE, FUKO BADO LIMEJAA MIHELA

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wachezaji wa timu ya Yanga kufunga mabao kadiri wanavyoweza, kwani ahadi yake ya kila bao shilingi milioni tano bado ipo hai kwa vile pesa zipo.

Akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka miwili ya uongozi wake, zilizoandaliwa na UWT, Rais Samia alisema aliona watu wakitania mitandaoni akimpigia simu Msigwa (Gerson, Msemaji wa Serikali) kuwa amwambie mwamuzi amalize mpira kwa kuwa hana fedha zaidi baada ya Simba kufunga bao la sita.

"Nataka niwahakikishie, pesa bado zipo, nyie wekeni mpira katika wavu, hela bado zipo."

Yanga inaingia dimbani usiku wa saa moja leo kuvaana na Monastr ya Tunisia na ushindi utaipeleka robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

No comments