MVUA KUBWA YATABIRIWA LEO NA KESHO

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema maeneo kadhaa katika baadhi ya mikoa itakuwa na mvua kubwa kiasi cha kuweza kusababisha madhara.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imesema, maeneo yatakayokumbwa na mvua hiyo ni katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi, Tabora, Kigoma, Singida, Dodoma na Ruvuma.

Tahadhari hiyo inasema madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua hizo kubwa ni pamoja na mafuriko na kukatika kwa mawasiliano ya baadhi ya sehemu na hivyo kusitisha kwa muda shughuli za uchumi.

No comments