KANISA LAPIGWA STOP KUENDESHA SHUGHULI ZAKE DAR ES SALAAM

Serikali, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndiyo inayosajili taasisi za kiraia na kidini, imelipiga stop kanisa moja kuendelea na shughuli zake jijini Dar es Salaam.

Askofu wa Kanisa hilo la Spirit Word Ministry, lenye makao yake eneo la Stakishari, Ukonga, Dkt Ceaser Masisi, alisema amepokea maelekezo hayo akitakiwa kusitisha huduma za kiroho hadi hapo watakapopewa maelezo zaidi.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia akaunti yake katika mitandao ya kijamii, askofu huyo alisema kwa sababu hiyo, wanawataarifu waumini wao katika kanisa hilo na matawi yake.

Hata hivyo hakugusia kuhusu sababu ya serikali kuchukua hatua hiyo.

No comments