BAKHMUT IMEZINGIRWA, KUTEKWA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA

Wapiganaji wa kukodi wa kundi la Wagner linalopigana sambamba na majeshi ya Russia katika vita vyake na Ukraine, wameuzingira mji wa Bakhumut na inasemekana wakati wowote kutoka sasa, watauteka na kuudhibiti.

Alexander Syrsky ambaye ni Kamanda wa Vikosi vya Ardhini wa jeshi la Ukraine, amesema wapiganaji wa kundi hilo wameuzingira mji huo kila upande na wanaendelea na majibishano makali ya mabomu na makombora, lakini kuna kila dalili za wao kuushika mji huo.

Alisema hadi wiki iliyopita, majeshi ya Russia yalikuwa yamekamata asilimia 50 ya mji huo na kila siku wanazidi kusogea kuuteka kabisa hali itakayowawezesha kusonga mbele zaidi katika wilaya zingine.

No comments