MARUFUKU VIONGOZI RUSSIA KUTUMIA iPhone

Wakati joto la vita kati ya Urusi na Ukraine halionyeshi dalili ya kupoa, maagizo mapya kutoka Klemlin, Ikulu ya Vladimir Putin, imewataka maofisa na viongozi wote wa serikali, kuachana na matumizi ya simu za mikononi za iPhone.

Taarifa iliyotolewa na ikulu imesema simu hizo zinazotengenezwa na kampuni ya Apple ya Marekani, zinaweza kutumiwa kwa kudukuliwa na kupata taarifa za mwenendo wa nchi hiyo, jambo ambalo ni hatari kwa usalama.

Wameambiwa hakuna ofisa yoyote wa serikali atakayeruhusiwa kutumia simu hizo ifikapo April, japo hakujatajwa simu mbadala.

Duru za kijasusi za nchi hiyo zinasema upo uwezekano wa simu hizo kudukuliwa na hivyo kujua mwenendo wa taifa hilo, hasa wakati huu wa mgogoro baina yake na nchi za Ulaya na Marekani.

No comments