AFISA USTAWI WA JAMII APIGWA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 13

Frank Mabuga ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 13.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kigoma, Eva Mushi, kwenye hukumu iliyosomwa kwa dakika 29 katika Chamber Court (chumba cha siri), alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 19, 2021 katika Nyumba ya Kulala wageni ya Ishimwe, iliyopo Kigoma Ujiji.

Alisema Mabuga alimbaka mtoto huyo mara mbili, hali iliyomsababishia maumivu makali pamoja na michubuko katika sehemu zake za siri.

Credit: Clouds fm

No comments