MAKAMO WA RAIS MAREKANI KUZURU NCHINI MWEZI HUU

Makamo wa Rais wa Marekani, Kamala Harris atazuru nchini baadaye mwezi huu, ikiwa ni mojawapo ya nchi tatu ambayo kiongozi huyo namba mbili atatembelea.

Harris ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya makamo wa rais katika historia ya Marekani, kama ilivyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais katika Afrika Mashariki.

Wanawake hao wawili walikutana mwezi uliopita wakati wa mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani uliofanyika huko New York.

Haijaeleweka bado nini hasa ajenda ya ziara hiyo, ingawa ni wazi kuwa suala la demokrasia litachukua nafasi kubwa hasa kwa siasa za maridhiano zinazoendelea hivi sasa nchini.

No comments