MFANYAKAZI WA BOA BENKI APIGIWA SIMU AKIWA KANISANI, AWAFUATA WAUAJI, WAMCHOMA MOTO KIBAHA

Neema Towo au Martha, mwenye umri wa miaka 30 ameuawa na watu wasiojulikana kwa kuchomwa moto kwa mafuta yanayodhaniwa ni petroli baada ya kupigiwa simu akiwa kanisani KKKT Kibaha, akatoka na kuwafuata wauaji waliokatiza uhai wake.

Kwa mujibu wa baba wa marehemu, mwanaye ambaye alikuwa akifanya kazi Benki ya Boa tawi la Kahama, aliuawa baada ya kumwagiwa mafuta ya petroli na pia kuchomwa sindano ambayo anadai ilienda kuharibu figo zake.

Alisema hata hivyo mtoto wake alipambana hadi mauti yake kwani akiwa amechomwa moto huo, alikimbia hadi kwa majirani zake ambako aliwapa namba yake ya simu ambao walimpigia na kumtaarifu juu ya tukio hilo.

No comments