RAIS WA CHINA AWASILI URUSI, APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE
Rais Xi Jimping wa China amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Nnukovo na kupokewa na mwenyeji wale Vladimir Putin.
Ziara ya Jimping ambayo inaangaliwa kwa umakini na nchi za Magharibi, haitoi nafuu kwa Ukraine, ambayo imevamiwa na Urusi kiasi cha mwaka mmoja uliopita na China imekataa kulaani uvamizi huo.
Hata hivyo China bado ina uhusiano mzuri na nchi hizo mbili huku ikitarajiwa pia kuwa kiongozi huyo wa Kikomunisti anaweza kusaidia kumaliza mzozo huo.
Rais wa Ukraine, Volodymryr Zelensky amesema anaamini China haitaipatia silaha Urusi ambayo hadi sasa imeteka miji kadhaa na haitegemewi kama itaondoka hivi karibuni.
China ni mshirika wa karibu wa Urusi kwa miaka mingi na nchi nyingi za Magharibi pamoja na Marekani zinaamini nchi hiyo inaweza kuipatia silaha Urusi ambayo imewekewa vikwazo na Ulaya.

Post a Comment