ZITTO AWA WA KWANZA KUMLIPA MAMA, ACT HAITASIMAMISHA MGOMBEA 2025

 

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekuwa wa kwanza kulipa fadhila za maridhiano kati ya Serikali na vyama vya upinzani, baada ya kutangaza kuwa hatagombea katika Uchaguzi Mkuu ujao na badala yake atafanya hivyo mwaka 2030.
Katika andiko lililopatikana kwenye mtandao wake wa kijamii, Zitto alisema kwa heshima waliyopewa, wao kama ACT wameamua kumlipa kwa kutosimamisha mgombea wakati huo, akisema badala yake watawekeza nguvu kubwa katika kuwapata wabunge wengi, ili wawe chama kikuu cha upinzani bungeni, ambacho wabunge wake hawatasusia Bunge la Katiba.



Akiwa katika kongamano la siku ya wanawake duniani Machi 8 mwaka huu mjini Moshi, Rais Samia aliwaambia wanachama wa Chadema kuwa hawaoni wakiwa na dhamira ya kutaka kusimamisha mgombea katika uchaguzi wa mwaka 2025 kwa kile alichosema, wanaamini mama yupo.
Hata hivyo, Chadema hawajasema chochote kuhusiana na kusimamisha au kutosimamisha mgombea katika uchaguzi ujao.

No comments