SAPRAIZ YA PETE KWA MCHUMBAKE NUSURA IMTOE UHAI

Maisha ya kisasa yanashika kasi sana katika jamii ya watu wa Afrika, wengi wakichukua staili ya maisha barani Ulaya.

Kijana mmoja nchini Kenya kutoka Kaunti ya Tana River aitwaye Johanna Charo, alijikuta akinusurika kumpoteza mpenzi wake siku ya kumposa, baada ya pete ya uchumba aliyoificha kwenye pilau kama sapraiz, kumezwa na mwanadada huyo!

Jessica Hawayu, binti ambaye alikuwa amefuatwa nyumbani na mchumba wake, hakuwa akijua kuwa familia yake, ikiongozwa na mama yake, walipanga na mchumba wake kumwekea pete hiyo ili impe sapraiz.

Lakini familia hiyo haikuamini wakati binti huyo alipoanza kuhangaika baada ya kuibugia pete hiyo katika tonge la pilau na hivyo kumfanya baba yake mzazi, ambaye pia aliujua mpango huo, alipompiga piga mgongoni na kumwezesha kuitema.

No comments