GIRL FRIEND WA TIGER WOODS ADAI FIDIA YA BILIONI 70 BAADA YA KUACHWA
Ericca Herman, binti ambaye amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na nyota wa Gofu duniani, Tiger Woods, amefungua shauri mahakamani akitaka kulipwa dola milioni 30 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 70, kama fidia baada ya kuachwa.
Ericca, aliyeishi na Woods kwa miaka sita, alisema katika shauri hilo kuwa mpenzi wake huyo na watu wake, walimtaka kufungasha vitu vyake kwa ajili ya safari fupi, lakini akaishia kutelekezwa uwanja wa ndege na akatakiwa kutorejea tena nyumbani.
Huko nyumbani, Woods alibadilisha vitasa vyote vya mlango na hivyo kumzuia msichana huyo kurejea katika nyunba ambayo anasema awali, walikubaliana kwa mdomo kuwa ataishi kwa miaka mitano bure endapo wataachana.

Post a Comment