GODBLESS LEMA AWATOA POVU OLE SENDEKA, DANIEL CHONGOLO

Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amemtolea uvivu aliyewahi kuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema juu ya kuhamishwa kwa kituo cha kuuzia madini ya Tanzanite, kilichopo Mirerani.

Machi 4 mwaka huu, akiwa na waandishi wa habari jijini Arusha, Lema alisema kituo cha kuuza madini ya Tanzanite hakipaswi kuwepo Mirerani pekee, akitaka kiwepo pia mjini Arusha.

Lakini Ole Sendeka, mwanasiasa machachari na wa siku nyingi kutoka chama tawala, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chomgolo, amesema Lema anadandia treni kwa mbele kwani soko la madini hayo adhimu, haliwezi kuhama Mirerani.

Alisema mwanasiasa huyo wa upinzani anatapatapa baada ya kurejea nchini akitokea uhamishoni Canada, kwani awali aliwatusi vijana wanaojitafutia riziki kihalali kwa kuendesha pikipiki, maarufu kama bodaboda.



Kwa upande wake, Chongolo alisema si kazi ya CCM kubishana na wanasiasa, bali kazi ya chama hicho ni kutafuta suluhisho la matatizo ya wananchi.


No comments