URUSI YAWAPONGEZA KENYA KUKATAA AJENDA YA USHOGA TOKA NCHI ZA MAGHARIBI
Urusi imeipongeza serikali na wananchi wa Kenya kwa kupaza sauti na kupinga uamuzi wa Mahakama ya Juu nchini humo kubariki ndoa za jinsia moja, ikisema kuna mkono wa mataifa ya magharibi na Marekani.
Katika akaunti ya Twitter ya ubalozi wa Urusi nchini Kenya, iliandikwa kwamba uharibifu huo wa maadili unaoletwa na nchi za magharibi ni mwanzo tu kwani kuna vitu vingi zaidi vitaletwa ambavyo vitaharibu utu wa mtu.
Mahakama ya Juu wiki iliyopita ilitoa hukumu ya kuruhusu ndoa za jinsia moja, uamuzi uliomshangaza Rais William Ruto ambaye aliapa kwamba jambo hilo halitatokea katika taifa hilo la Afrika Mashariki linalotajwa kuwa ndilo lenye demokrasia zaidi katika eneo hilo.
Ruto alisema pamoja na kuiheshimu mahakama, lakini Kenya ni nchi yenye katiba, sheria, mila, desturi na utamaduni wake hivyo haitaruhusu ndoa ya wanawake watupu au wanaume watupu.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda pia amepiga marufuku uhusiano wa jinsia moja na sheria inaenda kutungwa ya kifungo cha maisha kwa watakaokutwa na hatia ya kushiriki ndoa hizo

Post a Comment