MAREKANI HAIPO TOP TEN YA AIRPORT KALI DUNIANI, AFRIKA KUSINI INA VINNE TOP TEN AFRIKA
Licha ya ukweli kwamba Marekani ndilo taifa lenye uchumi imara zaidi duniani, lililoendelea katika nyanja karibu zote, lakini unapozungumzia viwanja vikali vya ndege, vya kisasa, haimo katika Kumi Bora duniani.
Kwa mujibu wa ripoti ya kitafiti iliyotolewa na BBC, kiwanja cha ndege kizuri zaidi na kinachoshika namba moja ni kile cha Changi (pichani) ambacho kinapatikana huko Singapore.
Kiwanja cha ndege kinachofuatia kwa ubora ni kile cha Hamad International Airport cha Doha (pichani) ambacho mwa miaka miwili iliyopita kilikuwa kikiongoza.
Katika Top Ten ya viwanja hivyo duniani ni namba tatu Haneda (Tokyo), Icheon (Seoul), Charles De Galle (Paris), Instanbul, Munich, Zurich, Narita (Tokyo) na Barajas huko Madrid.
Barani Afrika, nchi zinazofahamika kuwa na uchumi mkubwa kama Misri, Libya, Tunisia na Algeria, hazimo katika orodha ya viwanja bora kumi vya ndege.
Afrika Kusini ambayo ndiyo yenye miundombinu bora zaidi kati ya nchi zote za Afrika, inaongoza kwa kuwa na viwanja vya ndege vinne kati ya Kumi Bora.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town (pichani) ndio unaokamata namba moja, ukifuatiwa na ule wa Durban wa King Shaka na kumalizia tatu bora, uwanja wa Johannesburg.
Viwanja vingine vya ndege bora Afrika nafasi ya nne inaenda Casablanca, Mauritius, Marrakech, Addis Ababa, Kigali, Nairobi na wa kumi ni Bloefontein wa Afrika Kusini.

Post a Comment