ALLY MAYAI TEMBELE ATOBOA JUMUIA YA MADOLA
Kiungo wa zamani wa Yanga na Nahodha wa yimu ya Taifa, Taifa Stars, Ally Mayai ameteuliwa kuwa Mjumbe katika Bodi ya Ushauri wa Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Advisory Body on Sport –kwa kipindi cha miaka mitatu.
Hatua hiyo inatokana na kuimarika kwa nchi yetu katika nyanja za diplomasia ikiwemo ya michezo katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Uteuzi huo umefanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pindi Chana. Mayai ataiwakilisha Tanzania katika Bodi ya CABOS na kuwa Mjumbe mwakilishi wa Bara la Afrika.
Kwa sasa ndiye Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo nchini. Kiuzoefu Mayay ni mwanamichezo nguli na Nahodha mstaafu wa Timu ya Taifa ya (Taifa Stars) na ni kocha wa mpira wa miguu kitaaluma.
CABOS ni chombo cha kumshauri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Serikali wanachama kuhakikisha kunakuwepo ushirikishwaji thabiti wa Serikali na uwakilishi katika maendeleo ya sera na utekelezaji wake kwa kuzingatia maadili na matarajio yaliyowekwa ndani ya Mkataba wa Jumuiya hiyo.
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), anampongeza Bw. Mayay na kumtakia uekelezaji mwema wa majukumu yake.

Post a Comment