YANGA HAIZUILIKI LIGI KUU TANZANIA BARA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga hawazuiliki. Katika mechi yao ya leo dhidi ya Namungo, miamba hiyo ya Kariakoo, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, na kuwafanya kuendelea kupata baridi kileleni mwa msimamo.

Yanga ambayo sasa imefikisha pointi 59, ilipata bao la kwanza kwa mlinzi wake wa kati, Dickson Job kupiga kichwa safi kufuatia kona iliyochongwa na beki wake wa kulia, Djuma Shaaban.

Kipindi cha pili, kosa la kipa mkongwe, Dida, lilimpa nafasi kiungo Mburkinabe, Stephan Aziz Ki kufunga bao la pili na kupeleka shangwe kwa mashabiki kote nchono.

No comments