MBUNGE WA ZAMANI MBINGA AFARIKI
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mbinga, Timoth Lelanika Ndunguru mwenye umri wa miaka 92, amefariki dunia.
Mtoto wa marehemu, Emily Ndunguru ameiambia Ojuku Blog kuwa baba yake alifariki leo asubuhi, akiwa nyumbani kwake, Kibaha mkoani Pwani.
Emily amesema, mwili wa baba yake unatarajiwa kusafirishwa Jumatatu jioni kupelekwa Mbinga kwa mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika Jumatano katika Makaburi ya Mtakatifu Alois.
Marehemu aliyeoa mke mmoja nakupata naye watoto nane, ameacha wajukuu 32.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIDIMIWE

Post a Comment