OVANS CONSTRACTION YALA SHAVU MBINGA

Kampuni ya Ujenzi ya 

Ovans Construction Ltd ya mjini Mbinga imerundikiwa sifa lukuki kutoka kwa viongozi wa kiserikali wilayani hapa kutokana na ufanyaji kazi wake ulio bora.

Aliyeongoza pongezi hizo ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza 

Mwangosongo ambaye aliisifu kwa kuitikia wito wa kusaidia mafunzo ya awali ya ukandarasi kwa vijana 17 kutoka vikundi vitatu mjini hapa.

DC Aziza alisema Ovans ilichangia shilingi milioni tano ya ada ya wahitimu hao, waliopata ujuzi kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi ya jjini Mbeya.



Mkurugenzi Mtendaji wa Ovans Const. Ltd, Valence Urio, kushoto akiwa na Meneja wa Tarura Wilaya ya Mbinga Bwana Oscar



Wengine waliotoa sifa kwa kampuni hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbinga, ambaye alisema kampuni hiyo inafanya kazi nzuri kiasi kwamba wao hawana haja ya kutafuta mkandarasi mwingine, kwani Ovans wamethibitisha pasipo na shaka kwamba, wao ni watendaji kazi.

Alisema kazi wanazozifanya ni bora na zinazopaswa kuungwa mkono kwa kupewa kazi zaidi.




No comments