WATU 30 HUUAWA KWA RISASI KILA SIKU NCHINI AFRIKA KUSINI

Tàasisi isiyo ya Kiserikali ya Gun Free South Africa imesema kuwa takriban watu 30 huuawa kwa kupigwa risasi kila siku nchini Afrika Kusini.

Katika ripoti yake, taasisi hiyo imesema jumla ya watu 7000 wameuawa ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita, ikijumuisha mauaji ya watu wengi yaliyotokea jijini Johannesburg.

Rapa AKA aliyeuawa wiki iliyopita, amefanyiwa hivyo takriban miezi miwili tu baada ya DJ mmoja maarufu nchni humo, Sumbody naye kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake huko Johannesburg.

Mwanamuziki mwingine maarufu duniani, Lucky Dube naye aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake miaka michache iliyopita.

Rekodi hizo zimesema matukio hayo yamefikia kiwango hicho katika miaka ya karibuni.

No comments