MAREKANI YATUNGUA PUTO LA TATU, YATOA TAHADHARI

Marekani imetungua kifaa kisichoeleweka kilichokuwa kikielea katika anga lake, ambacho kimefanana na puto, ikiwa ni mara ya tatu ndani ya siku kumi.

Rais Joe Biden alitoa amri ya kutunguliwa kwa kifaa hicho kilichokuwa juu ya anga la nchi yake, wakati huu ambako nchi hiyo na Canada, imetoa tahadhari kwa wananchi wao wakati huu ambao dunia ipo katika changamoto kubwa ya usalama.

China ambayo puto lake la kwanza lilitunguliwa Februari 4 mwaka huu, likidaiwa kuchukua taarifa za kijasusi katika nchi zaidi ya 40, haijasema lolote hadi sasa.

No comments