NDEGE YAANGUKA KAHAMA,YAZUA TAHARUKI, POLISI, DC WATOA TAARIFA
Ndege ndogo binafsi, iliyodaiwa kusafiri ikitokea Rwanda kuelekea Msumbiji ikipitia Dar es Salaam imeanguka wakati ikitaka kutua kwa dharura katika uwanja mdogo wa mjini Kahama.
Taarifa zinasema katika ajali hiyo, watu kumi wanasadikika kupoteza maisha huku 32 wakipata majeraha. Ndege hiyo ilikuwa na abiria.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi wilayani humo limekanusha taarifa hizo, likisema kuwa hakukuwa na ajalo yoyote, bali kilichotokea ilikuwa ni mazoezi ya utayari wa vyombo vya uokoaji kupambana na majanga kama hayo.
Limesema mazoezi hayo yalihusisha jeshi la uokoaji, polisi na mamlaka za viwanja vya ndege na kwamba katika zoezi hilo, hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Kauli kama hiyo ilitolewa pia na Mkuu wa Wilaya, Mboni Mhita.

Post a Comment