WANAJESHI SABA WAHUKUMIWA KIFO KWA UOGA

Wanajeshi saba wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), wamehukumiwa kinyongwa hadi kufa baada ya kuthibitika kuwa walikimbia kutoka mstari wa mbele katika vita dhidi ya waasi wa M23.

Mahakama ya Kijeshi imewahukumu askari hao kwa kitendo chao hicho olichodai kilisababisha taharuki kwa wananchi na vifo vya raia kafhaa.

Askari hao walikimbia huku wakipiga risasi hovyo wakiwakimbia waasi hao ambao hivi sasa wanadaiwa kuukaribia mji wa Goma.

No comments