HECHE ASHANGAA WABUNGE KULIPWA KWA MKUPUO, WASTAAFU KIDOGOKIDOGO
Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche, ameshangazwa na kitendo cha wabunge kushindwa kuwatetea wastaafu wanaolipwa pesa zao kidogo kidogo, wakati wao wakilipwa kwa mkupuo.
Akizungumza jijini Dodoma jana, Heche ambaye amewahi kuwa mbunge wa Tarime, alisema wawakilishi hao wa wananchi ni wabinafsi, wasiotaka kuibana serikali kurekebisha sheria ya kikokotoo, kwa kuwa wao haiwahusu.
Alisema baada ya miaka mitano ya uwakilishi bungeni, wabunge hulipwa shilingi milioni 250 kwa mpigo, wakati wastaafu hupewa kidogokidogo, kitu kinachowafanya washindwe kutimiza malengo yao.
"Wabunge wanatakiwa kuwatetea wastaafu, siyo wanakaa tu na kuzunguka kwenye viti pale bungeni," alisema.

Post a Comment