WAFUNGWA 40,000 WENYE TATTOO WADHIBITIWA EL SALVADO

Genge linaloendesha shughuli za uhalifu nchini El Salvador, ambalo wanachama wake wamejichora mwilini, wanakamatwa na kuhifadhiwa katika gereza moja ambalo hadi sasa, idadi ya wafungwa inafikia 40,000.

Rais Nayib Bukele wa El Salvador anasimamia ukamatwaji wa wanachama wa genge hilo ambalo linaendesha mauaji na vitendo vingine vya kihalifu nchini humo.

Kundi kubwa la wafungwa, wakiwa na pingu mikononi, kifua wazi na hawana viatu, walionekana wakiingizwa katika gereza kubwa zaidi nchini humo na wote walionekana wakiwa  na michoro katika miili yao.

No comments