MWANA FA ATEULIWA NA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Mbunge wa Muheza ambaye pia ni msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya,Hamis Mwijuma anayefahamika zaidi kama Mwana Fa, ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Mkali huyo wa muziki wa kufokafoka, ni miongoni mwa wanasiasa kadhaa ambao wameteuliwa kuchukua nafasi mbalimbali kama Uwaziri, Manaibu Mawaziri na wakuu wa mkoa.

No comments